Nenda kwa yaliyomo

Busta Rhymes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Busta Rhymes

Busta mnamo 2022
Amezaliwa Trevor George Smith Jr.
20 Mei 1972 (1972-05-20) (umri 54)[1]
New York City, Marekani
Nchi Marekani
Majina mengine Trevor Taheim Smith
Kazi yake Rapa, mwongozaji wa filamu, mtayarishaji wa muziki, mwigizaji
Mwajiri Conglomerate, Empire, Cash Money
Urefu 1.85 m
Kipindi 1986–sasa[2]
Dini Uislamu
Watoto 6
Tovuti bustarhymesuniverse.com

Trevor George Smith Jr. (amezaliwa Mei 20, 1972), anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama Busta Rhymes, ni rapa, mtayarishaji wa muziki, mwongozaji wa filamu, na mwigizaji mashuhuri kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa uwezo wake wa kipekee wa kuchana kwa kasi ya ajabu na kutumia vionjo vya hali ya juu katika video zake. Busta amepokea jumla ya teuzi 12 za Grammy Award, jambo linalomfanya kuwa mmoja wa wasanii walioteuliwa mara nyingi zaidi bila kushinda tuzo hiyo. Majarida ya Billboard na Vibe yamemtangaza kuwa mmoja wa marapa 50 bora wa muda wote.[3][4]

Alianza safari yake ya kimuziki kama mwanachama wa kundi la Leaders of the New School, ambalo lilipata umaarufu mkubwa likiwa kwenye ziara na kundi la Public Enemy.[5] Baada ya kundi hilo kusambaratika, Busta alijizolea sifa kama msanii wa kujitegemea na kutoa albamu yake ya kwanza, The Coming (1996), ambayo ilishika nafasi za juu kwenye chati na kutunukiwa cheti cha platinamu. Busta Rhymes pia ni mwanzilishi wa lebo ya muziki ya Conglomerate na kundi la Flipmode Squad.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Trevor George Smith Jr.[6] alizaliwa katika kitongoji cha East Flatbush huko Brooklyn, New York City, mnamo Mei 20, 1972. Wazazi wake, Geraldine Green na Trevor Smith Sr., walikuwa wahamiaji kutoka nchini Jamaika.[7]

Alipofikisha umri wa miaka 12, familia yake ilihama kutoka Brooklyn na kwenda kuishi Uniondale, New York huko Long Island. Busta alipata fursa ya kusoma katika shule ya ufundi ya George Westinghouse Career and Technical Education High School iliyopo Brooklyn pamoja na magwiji wa baadaye wa Hip hop kama The Notorious B.I.G. na Jay-Z.[8] Hatimaye, alihitimu elimu yake ya sekondari katika shule ya Uniondale High School mwaka 1991.[9]

Mbali na maisha yake ya Marekani, Busta pia aliwahi kuishi nchini Uingereza mwanzoni mwa miaka ya 1980 akiwa na shangazi yake upande wa mama huko Morecambe. Katika mahojiano yake na jarida la GQ mwaka 2020, alieleza kuwa kipindi hicho alihudhuria shule nchini Uingereza na alikuwa akicheza "mabreka" kwenye klabu mbalimbali akiwa mdogo.[10]

Kazi ya muziki

[hariri | hariri chanzo]

1986–1995: Leaders of the New School

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 1986, Busta akiwa na wenzake waliunda kundi la Leaders of the New School. Walitoa albamu yao ya kwanza, A Future Without a Past..., mnamo Juni 1991 kupitia lebo ya Elektra Records. Kundi hilo lilipata umaarufu mkubwa zaidi baada ya kushirikishwa kwenye wimbo wa kundi la A Tribe Called Quest uitwao "Scenario".[11] Hata hivyo, kutokana na umaarufu wa Busta kuongezeka, kundi likavunjika rasmi wakati wa kipindi cha Yo! MTV Raps mwaka 1993.[12]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za studio

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za ushirikiano

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Monitor". Entertainment Weekly. Na. 1260. Mei 24, 2013. uk. 34.{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. John Bush. "Busta Rhymes". AllMusic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 14, 2019. Iliwekwa mnamo Novemba 23, 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Rouhani, Carl Lamarre, Gail Mitchell, Keith Murphy, Michael Saponara, Datwon Thomas, Mark Elibert, Eric Diep, William E. Ketchum III, Heran Mamo, Neena (2023-02-08). "50 Greatest Rappers of All Time". Billboard (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-03-08.{{cite magazine}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  4. Bossi, Andrea. "The 50 Top Rappers Of All Time". Forbes (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 10, 2024. Iliwekwa mnamo 2025-03-08.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Busta Rhymes Reunites On Stage With Leaders of the New School". HipHopDX.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 11, 2017. Iliwekwa mnamo Septemba 11, 2017.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Busta Rhymes must be released, orders judge". The Daily Telegraph. Iliwekwa mnamo Machi 23, 2016.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Bush, John (Mei 20, 1972). "Busta Rhymes Biography". AllMusic. Iliwekwa mnamo Aprili 25, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Reed, Ryan (Oktoba 21, 2015). "Jay Z Talks High School Rap Battle With Busta Rhymes on 'Kimmel'". Rolling Stone. Iliwekwa mnamo Septemba 24, 2020.{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Notable Long Islanders". Newsday. New York City / Long Island. Septemba 17, 2018. Iliwekwa mnamo Septemba 24, 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Coker, Cheo Hodari (Novemba 21, 2020). "The Voice: What Busta Rhymes Has Learned After over 30 Years in Hip-Hop". GQ.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Young, Kevin. "Unwrapping the Message". Bookforum. Iliwekwa mnamo Novemba 16, 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. Markman, Rob. "Busta Rhymes Recalls LONS' 'Yo! MTV Raps' Breakup". MTV. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-17. Iliwekwa mnamo Machi 24, 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)