Nenda kwa yaliyomo

Baasha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Baasha alivyochorwa mwaka 1553.

Baasha (kwa Kiebrania בַּעְשָׁא, Baʿšāʾ) alikuwa mwana wa [[Ahiya] wa kabila la Isakari akatawala kwa miaka 23 Ufalme wa Israeli baada ya kumuua mfalme Nadabu wa Israeli na kuangamiza familia yote ya Yeroboamu I kama alivyotabiri nabii Ahiya.

Biblia inamhukumu hasa kwa kuendeleza sera ya kidini iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi.

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Kwanza cha Wafalme, 15-16.

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Baasha kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.